Natambua fika kuwa sisi vijana
tunakumbana na matatizo mengi, tunazo changamoto nyingi zinazokwamisha kabisa
jitihada zetu za kufika kilele cha mafanikio. Changamoto hizo hupelekea baadhi
yetu kukata tamaa huku wakiamini kuwa mafanikio siyo sehemu ya maisha yao.
Lakini leo hii naomba sote kwa pamoja tuungane, tushikamane, tuongozane ili tu
kwa pamoja tufikie mafanikio tunayoyaota kila kukicha. Naomba tuamini kuwa
kesho hujengwa na leo na vijana ndiyo samadi ya
mafanikio katika taifa lolote lile.
Kwa nadharia kabisa vijana
tunaonekana tumesahaulika lakini kivitendo naomba niweke wazi vijana tumejisahau wenyewe na ndiyo sababu inayotufanya
tuendelee kuwa tegemezi. Hivyo leo nawaomba vijana
wenzangu tuamke na kwa nguvu zetu, kwa wepesi wetu na wingi wetu tushiriki
katika shughuli zote za maendeleo hasa zilizo
nyanja za kufanya maamuzi yanayotuhusu.
Kushiriki kwetu ndiko kutaondoa changamoto, kero, matatizo na vikwazo vya
mafanikio yetu katika nyanja zote za maendeleo.
Tufahamu kuwa maendeleo hayaletwi na mtu mmoja, “maendeleo ni matokeo ya kuunganisha nguvu za
watu, akili na ujuzi.” Ni wazi kuwa ushiriki wetu katika nyanja za maendeleo ni wa kubabaisha sana. Inawezekana kabisa
ushiriki wetu huu ndiyo ikawa chanzo cha sisi kuendelea kuwa tegemezi kwa kila
jambo. Pia inawezekana kabisa ushiriki huu mdogo na wa kubabaisha unasababishwa
na uoga kwa baadhi yetu huku wengine wakiamini muda wao bado haujafika.
Naomba niwatoe uoga vijana wenzangu na niwaase
kuwa kundi la vijana ndilo kundi pekee ambalo
linaweza kuleta mabadiliko chanya ya kifikira na si kundi jingine. Hivyo
tunalojukumu na wajibu wa kujitolea kuipigania nchi yetu dhidi ya wale wote
wasio na dhamira ya kweli. Na moja kati ya njia ya kizalendo na kishujaa ya
kuipigania nchi yetu ni kuomba dhamana ya uongozi kuanzia ngazi ya udiwani
mpaka ubunge badala ya kuendelea kulalamika kuwa watawala wa sasa hawatimizi
matakwa yetu ya kila siku.
Nia nyingine ya kizalendo na ya kishujaa ya kuihami nchi ni ile ya kushiriki
kikamilifu, kinadharia na kivitendo katika mchakato mzima wa uchaguzi kwa
kupigia kura vijana wenzetu ambao wamejitolea
dhamana ya kutaka kutuongoza kutoka hapa tulipo na kutupeleka kwenye nchi ya
mafanikio. Ndugu zangu, vijana wenzangu tuwaunge
mkono vijana wenzetu, tuwape nauli hiyo, tuwatume
wakatutumikie ili kesho tusijilaumu wenyewe. Naomba tukumbuke kuwa mafanikio
yetu ya kesho ni matokeo ya nguvu zetu tulizoziunganisha leo. Tushiriki katika
siasa ili tuongeze nguvu ya kutuamulia mawazo yetu wenyewe.
Na njia ya tatu na muhimu kabisa ni kushiriki kikamilifu na kwa ukaribu wa hali
ya juu katika mchakato mzima wa kuundwa kwa katika mpya. Ni haki yetu ya msingi
kabisa kushiriki na ni wajibu wetu kushiriki, kwani katiba ndiyo chombo ambacho
kitalinda haki zetu na uhuru wetu.
Ndugu zangu vijana, tutambue kuwa kudorora kwa
uchumi barani afrika kunatokana na kukosekana kwa nguvu kazi. Ushiriki wetu
katika shughuli za kiuchumi bado si wa kuridhisha sana kwani kiwango cha ajira
katika taasisi za serikali na zile za binafsi hakiridhishi sababu ni vijana wachache sana waliobahatika kuajiriwa huko. Wengi
ambao hawajapata bahati hiyo wao wamekimbilia katika shughuli za umachinga,
ukuli huku wakina dada wakiangukia kwenye shughuli za ubaa medi, kazi za ndani
na kazi zingine zisizo lipa kipato kizuri. Pia vijana
wengine huangukia katika udokozi, vibaka na ulevi wa madawa ya kulevya kwa
sababu ya kukosa kazi za kufanya.
Hali hii kiujumla inadumaza uchumi wa vijana wengi
sana kwani pamoja na juhudi zinazofanywa na wachache wetu lakini bado vitu kama
elimu duni, ukosefu wa mtaji wa kutosha na ukosefu wa vifaa vya uzalishaji bado
ni vikwazo kwa vijana na ni tatizo sugu
linalokwamisha maendeleo ya vijana
hasa katika nyanja hii ya uchumi pia ukosefu wa lishe bora kwa vijana na njaa pamoja na ukeketaji kwa wasichana bado ni
tatizo linalokwamisha maendeleo ya uchumi wetu na
wa taifa kwa ujumla. Na ili hili liweze kutatuliwa basi hatuna budi kama vijana kuongeza nguvu hasa sehemu za maamuzi muhimu
yanayogusa maisha yetu ya kila siku.
Ndugu zangu, vijana wenzangu, tukumbuke kuwa
pamoja na changamoto hizo zote zilizotajwa lakini kubwa zaidi ni hili la vijana kuwa waathirika wakubwa wa magonjwa hatari na
yasiyo na tiba. Magonjwa kama malaria, kifua kikuu na ukimwi yamekuwa tishio
hasa kwa vijana. Vijana
wengi tumejisahau na kuwa watumwa wa magonjwa hatarishi. Magonjwa haya ndiyo
yanayomaliza nguvu kazi yetu na kudumaza uchumi wetu. Inatakiwa ifike kipindi
sote kwa pamoja tutamke “UKIMWI SASA BASI, TUNATAKA MAENDELEO
ENDELEVU.”
Mwisho ndugu vijana wenzangu, hatuna budi kwa
wingi wetu, kwa wepesi wetu, kwa fikra zetu, kwa utashi wetu, kwa umri wetu na
kwa nafasi yetu tunaweza kabisa kuiandika historia mpya ya nchi yetu. Historia
itakayobadili kabisa misamiati ya lugha yetu, historia itayorudisha furaha yetu
iliyopotea miaka mingi iliyopita lakini historia hii haiwezi kuandikwa kwa uoga
na usaliti. Ni wazi tunatakiwa kuwa na mioyo ya kizalendo ambayo itatusukuma
kushiriki moja kwa moja katika kufanya maamuzi muhimu na magumu yahusuyo taifa
letu.
Niwazi kuwa miongoni mwetu tunahitaji tuwapate wakina Nyerere wengine, Salim
Ahmed Salim, Amina Chifupa wengine. Tunahitaji kuwaona watu kama James Mbatia
wengi miongoni mwetu. Tunahitaji kuwaona vijana
kama Martin Luther King, Malcolm X enzi za uhai wao, Abdulwaheed Sykes enzi za
TAA na TANU. Tunahitaji kuwapata wakina Halima Mdee, John Mnyika na Zito Kabwe
wengi katika taifa hili. Tunahitaji kupata vijana wenye muono wa mbali,
walio na moyo wa kuthubutu na waliotayari kulitetea na kulilinda taifa lao kwa
nguvu zao, kwa umri wao, kwa wingi wao, kwa utayari wao na hata kwa mawazo na
hoja zao.
Hatuwezi kuwapata vijana hawa kama hatutashiriki
kivitendo katika nyanja zote za maendeleo.
Hatuwezi kuwapata vijana hawa kama tutaendelea
kuogopa naomba tutambue kuwa “uoga katika mafanikio ni sawa na umasikini”
hatuwezi kuwapata vijana hawa kama tutaogopa
mabadiliko. Vijana tuamke, tushikamame tena
mshikamano thabiti, tushiriki na kuingia katika vyombo muhimu vya maamuzi kama
hatua ya kuuenzi ujana wetu na kuilinda nchi yetu.
Nawatakia kazi njema za kuendeleza na kukuza uchumi wetu.
Na. Muhsin siraji
0717664685
How do you make money in gambling? - WorkTime
ReplyDeleteHow do you make money in gambling? This method involves gambling 카지노 on your partner with a kadangpintar variety of different sports betting options How do you earn money with online gambling?What is the best งานออนไลน์ online casino?